USIJUE HILI: KARIAKOO !!!!!!UTAAMKA!!!!!
Kariakoo
Historia ya jina la kariakoo inaanzia tangu enzi za wa
mjerumani wakati wa Tanzania bara ikiitwa Tanganyika.
Mahala lilipo soko
palijengwa jengo na utawala wa Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama
ukumbi wa kuadhimishwa na kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim wa Ujerumani kwa
wakati huo.
Lakini mara tu baada ya jengo kukamilika, Vita kuu ya kwanza ya
dunia ilianza na Waingereza walipouteka mji wa Dar es Salaam, walilitumia jengo
hilo kama kambi ya jeshi kwa askari waliojulikana kama Carrier-Corps kwa jina
la kigeni, yaani wabebea mizigo likitafsiriwa kwa Kiswahili.
Shimoni kariakoo |
Jina hilo la
maaskari wabeba mizigo katika Kiswahili lilitamnkwa Kariakoo na liliendelea
kutumika kama jina la eneo lote linalozunguka mahala lilipo soko
la kariakoo.
KAMA UNA HISTORIA YA MA/JINA LA KIJIJI, MJI, WILAYA, MIKOA NA SEHEMU ZINGINE, WALIVYOYAITA TAFADHALI TUTUMIE kingsuka123@gmail.com
Kama unamaoni au kuboresha historia niliyoipost tafadhali tutumie kingsuka123@gmail.com au toa maoni yako mwishoni mwa post.
AHSANTE KWA KUSOMA POST:::::::::::::KARIBU TENA
Wakati wa Ujerumani nchi hii ilikuwa ikiitwa Deutsch Ostafrika, Tanganyika ilianza kutumika 1922
ReplyDelete